JINSI YA KUTUMA MAOMBI YA AJIRA ZA UALIMU 2020 KWA TOVUTI YA OTEAS




Habari watembeleaji wa blogu hii ya kielimu ya School PVH. Serikali kupitia wizara ya Tamisemi imetangaza ajira mpya za walimu wa shule za msingi na sekondarikwa mwaka 2020, 

MUHIMU KWA WAOMBAJI WOTE
Usajili wa waombaji
  1. Kila muombaji anatakiwa ajisajili kwa kuandika taarifa muhimu kama vile namba ya kidato cha nne, mwaka wa kumaliza, jina la muombaji, namba za simu na Barua ya barua pepe (email) inayojua kazi.
  2. Kila muombaji anatakiwa ajisajili mara moja tu. Mfumo hautahusu kufanya usajili na kutuma maombi zaidi ya mara moja.
  3. Hakikisha kila taarifa unaona jaza unaihakiki kabla ya kwenda kwa vitu vingine.
Taarifa binafsi
  1. Majina yatakayo jazwa sehemu ya taarifa ya kibinafsi kama yanavyoonekana katika vyeti vya taaluma.
  2. Namba ya mtihani wa kidato cha nne na sita iandikwe kwa muundo wa S0123-0001 au P0123-0001.Hakikisha namba unayo sahihi.
Utumaji wa nyaraka
  1. Unatakiwa kuambatanisha nyaraka kwa kila taarifa ya kitaaluma, leseni ya kazi na cheti cha kuzaliwa.
  2. Cheti kinacho tumwa hakikisha ukubwa mkubwa zidi MB 2.Inashauriwa kuscan cheti halisi inayoonekana vizuri.
  3. Barua ya maombi ielekezwe kwa KATIBU MKUU, OFISI YA RAIS, TAMISEMI. Unganisha barua ya maombi na barua ya INTERNSHIP
  4. Viambatanisho vyote vya nyaraka muhimu zinazohitajika katika mfumo wa kazi katika muundo wa PDF tu.


Utaratibu wa kutuma maombi ni kwa njia ya mtandao katika tovuti ya ONLINE TEACHING APPLICATION SYSTEM. Hivyo basi natoa maarifa yatakayokuwezesha katika mfumo huu na kujiunga kisha kutuma maombi yako ya ajira
JINSI YA KUFUNGUA AKAUNTI OTEAS
Kwa ambao bado hawakuwahi kujiunga na OTEAS inatakiwa kwanza wafungue akaunti kisha wataendelea na uombaji. zifuatazo ni hatua za kufuata ili ufungue akaunti yako OTEAS

Ingia katika tovuti ya OTEAS 👉  BOFYA HAPA   

Hapo itafunguka na kukuletea muonekano huu hapa chini kwenye picha,

Ikiwa tayari una akaunti utajaza USER NAME na PASSWORD zako utabofya SIGN IN lakin kwa wale ambao hawana akaunti inatakiwa wafungue akaunti na wanatakiwa kubofya hapo chini palipoandikwa YOU DON'T HAVE ACCOUNT CLICK HERE TO CREATE kama ilivoonyeshwa kwenye picha hapa chini


Baada ya kugusa sehemu hiyo ili kuanza kufungua akaunti yako ya OTEAS utaletewa muonekano huu kama unavyoonekana katika picha hapa chini


Hapa utatakiwa uanze kujaza taarifa zako zinazohitajika kama ulivoonyeshwa hapo kwenye picha jaza PASSWORD ambazo ni kuanzia namba au herufi nne na kuendelea na pia hakikisha unaweka PASSWORD ambazo hata badae utazikumbuka.

Jaza USER NAME hili ni jina lolote ambalo ni la kukutambulisha wewe na ni jina ambalo utalitumia kuingia kwenye akaunti yako kwahiyo andika jina ambalo utakua unalikumbuka mda wowote ukihitaji kuingia kwenye akaunti yako ya OTEAS.
Tazama 

Tazama picha hapo chini ikiopnyesha jinsi Mwalimu huyu alivojaza taarifa zake.


Na unapomaliza kujaza taarifa zako zote utabofya hapo palipoandikwa REGISTER. ukibofya hapo tayari utakua umekamilisha kujisajili na mfumo huu na itakuonyesha hivi tazama picha hapo chini.


Sasa umeshajiunga na OTEAS ukibofya OK itakurudisha sehemu ambayo utaweza kuingia SIGN IN kwenye akaunti yako ya OTEAS na kuanza kuomba ajira.

  JINSI YA KUOMBA AJIRA KWA MFUMO WA OTEAS

Ingia kwenye akaunti kwa kujaza USER NAME na PASSWORD zako kisha itafunguka na kukuletea muonekano huu hapa chini tazama picha.

Hakikisha unagusa vipengele vyote vya kushoto mwa picha hii vikianziwa na Personal information vijaze vyote na ukamilishe maelekezo kwa kila kipengele ndipo utagusa hapo APPLY FOR POST.


KWA MAELEZO ZAIDI TAZAMA VIDEO IFUTAYO


 👉👉TUMA MAOMBI HAPA

Pia soma hii 👇👇👇

Pia soma hii 👇👇
________________________________________