KISWAHILI || CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

Kozi hii ni miongoni mwa kozi kumi na tano (15) za mwaka mmoja katika mfululizo wa Programu ya Maandalizi (Foundation Programme). Kozi hii pia ni mojawapo ya kozi kwa wanafunzi wa Stashahada ya Ualimu wa Shule za Msingi (Diploma in Primary Teacher Education).

Madhumuni ya Kozi

Utakapomaliza kusoma kozi hii, utaweza: 

  1. Kueleza maana ya lugha na chimbuko la lugha ya Kiswahili.
  2. Kuunda tungo mbalimbali.
  3. Kuelezea muundo wa maneno ya Kiswahili.
  4. Kutambua kategoria za kisintaksia na ushahidi wa kuwepo kwazo
  5. Kuainisha sentensi za Kiswahili na kuzichanganua kwa njia mbalimbali
  6. Kutathmini fasihi ya Kiswahili kwa jumla