FASIHI KWA UJUMLA



FASIHI
Pia Huitwa
Sanaa ya Lugha
Kiingereza
Literature
Tanzu Kuu za Fasihi
Fasihi Simulizi
Fasihi Andishi
Ushairi*
Fasihi Simulizi
Hadithi
Nyimbo
Tungo Fupi
Maigizo
Fasihi Andishi
Riwaya
Hadithi Fupi
Tamthilia
Pia Angalia
Tamathali za Usemi

Prev
Lugha
Next
Insha

Fasihi ni sanaa ya lugha. Fasihi hutumia lugha kutoa sanaa mbalimbali katika jamii.
Tanzu za Fasihi
Kuna tanzu mbili kuu za fasihi, na kila utanzu una vipera vyake: Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi:
Fasihi Simulizi
  1. Hadithi (Ngano) - hekaya, mighani, visasili n.k
  2. Nyimbo - za jandoni, za ndoa, za kazi n.k
  3. Maigizo - michezo ya kuigiza, ngomezi n.k
  4. Tungo Fupi - methali, vitendawili n.k
Fasihi Andishi
  1. Hadithi Fupi - hadithi isiyokuwa ndefu iliyochapishwa katika mkusanyiko wa hadithi nyingine
  2. Riwaya - hadithi ndefu iliyochapishwa katika kitabu chake pekee
  3. Tamthilia - mchezo wa kuigiza uliowekwa kwa maandishi
  4. Ushairi* - mashairi yaliyoandikwa
Tofauti kuu kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi ni kwamba Fasihi Simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo au matendo ilhali Fasihi Andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.
Tanbihi:Ushairi ni kipera cha nyimbo lakini pia mashairi yanaweza kuwa chini ya Fasihi Andishi, ikiwa yamechapishwa.
Tofauti kati ya Fasihi Andishi na Fasihi Simulizi

FASIHI SIMULIZI
FASIHI ANDISHI
1.
Huwasilishwa kwa njia ya mdomo na/au matendo.
Huwasilishwa kwa njia ya maandishi
2.
Ni mali ya jamii.
Kazi andishi ni mali ya mwandishi (na mchapishaji)
3.
Msimulizi anaweza kubadilisha sehemu fulani
Kitabu kilichoandikwa hakiwezi kubadilishwa
4.
Huhifadhiwa akilini
Huhifadhiwa vitabuni
5.
Kazi simulizi hubadilika na wakati
Kazi andishi haibadiliki na wakati
6.
Huhitaji msimulizi na hadhira yake wawe mahali pamoja wakati wa masimulizi
Msomaji anaweza kusoma kitabu cha hadithi peke yake, mahali popote, wakati wowote
7.
Mtu yeyote anaweza kutunga na kusimulia
Ni lazima mwandishi na msomaji wawe na uwezo wa kusoma
8.
Hutumia wahusika changamano (wanyama, watu, mazimwi n.k)
Hutumia wahusika wanadamu.
Umuhimu wa Fasihi Katika Jamii
  • Kuburudisha jamii. Takribani vipera vyote vya fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na kusisimua hadhira.
  • Kuelimisha. Fasihi hukusudia kuelimisha hadhira kuhusu jamii, mazingira n.k
  • Kudumisha maadili katika jamii kwa kuelekeza, kuonya na kunasihi hadhira jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii.
  • Kuunganisha jamii. Fasihi huleta pamoja watu katika jamii. Kwa mfano, katika nyimbo, miviga, vichekesho.
  • Kukuza lugha. Aghalabu tungo zote za fasihi hutumia lugha. Isitoshe, fasihi hutumia mbinu nyingi za lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na ukwasi wa lugha.
  • Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii. Aghalabu kazi za fasihi (hasahasa Fasihi Simulizi) huambatanishwa na desturi mbalimbali za jamii husika.
  • Kukuza uwezo wa kufikiri. Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri sana ili kupata suluhisho. k.m vitendawili, ngano za mtanziko n.k

Fasihi Simulizi
FASIHI SIMULIZI
Utanzu wa
Fasihi
Kiingereza
Oral Literature
Tanzu za Fasihi Simulizi
Hadithi / Ngano
Nyimbo
Maigizo
Tungo Fupi

Prev
Tamathali za Usemi
Next
Fasihi Andishi
VIPERA VYA TANZU ZA FASIHI SIMULIZI
HADITHI / NGANO
Khurafa
Hekaya
Mighani / Visakale
Usuli / Visaviini
Visasili
Hadithi za Mtanziko
Hadithi za Mazimwi
NYIMBO
Mashairi
Kimai
Wawe/Hodiya
Nyimbo za Ndoa
Nyimbo za Kidini
Nyimbo za Kisiasa
Za Tohara/Jandoni
Nyimbo za Kizalendo
TUNGO FUPI
Methali
Vitendawili
Mafumbo
Vitanza Ndimi na Vichezea Maneno
Semi
Lakabu
Misimu
MAIGIZO
Michezo ya Kuigiza
Ngomezi
Miviga
Malumbano ya Utani
Mazungumzo/Soga
Ulumbi
Vichekesho
Maonyesho

Fasihi Simulizi ni utanzu wa fasihi ambao unawakilisha sanaa ya lugha inayopitishwa kutoka kwa kizazi hadi kizazi kwa njia ya maneno/masimulizi ya mdomo.
Sifa za Fasihi Simulizi
  1. Hupitishwa kwa njia ya mdomo
  2. Ufanisi wa sanaa katika fasihi simulizi hutegemea uwezo wa msimulizi, au wahusika
  3. Masimulizi yake yanaweza kuathiriwa na mazingira, hisia na hali
  4. Ni mali ya jamii. Hakuna mtu fulani anayemiliki sanaa katika fasihi simulizi.
  5. Inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, au mazingira mbalimbali kwa sababu hutegemea kumbukumbu ya msimulizi.
  6. Aghalabu huwa na funzo fulani
Umuhimu wa Fasihi Simulizi
  1. Kuburudisha - Hufurahisha na kuchangamsha hadhira
  2. Kunasihi- kutolea mawaidha na kuonyesha mwelekeo unaotarajiwa katika jamii
  3. Kuelimisha watu kuhusu vitu mbalimbali hasa mazingira yao
  4. Kutambulisha jamii - jamii mbalimbali husifika kutokana na sanaa zao katika fasihi simulizi kama vile nyimbo
  5. Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii
  6. Kuunganisha watu - huleta watu pamoja
  7. Kukuza lugha - fasihi huimarisha lugha kwa kuwa hutumia mbinu mbalimbali za lugha.
  8. Kuliwaza - hutoa huzuni na kuleta matumaini.
  9. Kupitisha muda - wakati mwingine fasihi simulizi hutumika kupitisha muda.


Fasihi Andishi
FASIHI ANDISHI
Utanzu wa
Fasihi
Kiingereza
Written Literature
Tanzu za Fasihi Andishi
Hadithi Fupi
Riwaya
Tamthilia
Ushairi - Mashairi Yaliyoandikwa
Angalia
Aina za Wahusika
Hadithi Fupi vs Riwaya
Tamathali za Usemi

Prev
Fasihi Simulizi
Next
Ushairi

Fasihi Andishi ni aina ya sanaa ambayo hutumia maneno yaliyoandikwa kupitisha ujumbe. Ni sanaa inayopitishwa kwa njia ya maandishi
Tanzu za Fasihi Andishi
Kuna tanzu nne kuu za Fasihi Simulizi:
  1. Hadithi Fupi - kazi andishi ya fasihi isiyokuwa ndefu sana
  2. Riwaya - kazi andishi ya fasihi ambayo huwa ndefu kuliko hadithi fupi
  3. Tamthilia- kazi andishi ya fasihi inayowasilisha mchezo wa kuigiza
  4. Mashairi - mashairi yaliyochapishwa huwa chini ya fasihi andishi.
Sifa za Fasihi Andishi
  1. Hupitishwa kwa njia ya maandishi
  2. Ni mali ya mtu binafsi
  3. Haiwezi kubadilishwa
  4. Hutumia mbinu za lugha na mbinu za sanaa
Umuhimu wa Fasihi Andishi
  1. Kuhifadhi kazi ya sanaa katika maandishi
  2. Kukuza lugha
  3. Kuburudisha
  4. Kuelimisha
  5. Kukashifu tabia zisizoandamana na maadili ya jamii
  6. Kuonya, kuelekeza, kunasihi
Uchambuzi wa Fasihi Andishi
Unapochambua kazi ya fasihi andishi zingatia:
Aina ya Kazi Andishi
  • Tambua aina au kipera cha kazi andishi ikiwa ni riwaya, hadithi fupi au tamthilia
Wahusika
  • Tambua wahusika katika kazi hiyo ya fasihi
  • Fafanua sifa za kila mhusika kwa kutumia vivumishi au virai vivumishi vinavyolingana na hulka za mhusika huyo.
  • Aidha, unapaswa kuyakinisha sifa hizo kwa kutolea mifano kutoka kwenye hadithi
  • Taja aina ya wahusika
Maudhui na Dhamira
  • Maudhui - ni nini kinachofanyika?
  • Dhamira - lengo/kusudi la kazi hiyo ni nini?
Mandhari
  • Hadithi inafanyika katika mazingira gani?
  • Mazingira hayo yanachangia vipi katika kisa hicho au sifa za wahusika?
  • Msanii ameunda hali gani? (hisia, n.k)
Mbinu za Lugha
  • Taja kwa kutolea mifano, fani za lugha zilizotumika ili kuifanya lugha iwe ya kuvutia zaidi
  • Fafanua mbinu za sanaa zilizotumika na utaje mifano mwafaka

Ushairi
USHAIRI
Utanzu wa
Fasihi
Nyimbo
Fasihi Andishi
Kiingereza
Poetry
Tutaangazia
Aina za Mashairi
Bahari za Ushairi
Uchambuzi wa Mashairi
Maghani

Prev
Fasihi Andishi
Next
Tamathali za Usemi

Ushairi ni utungo wa kisanaa unaotumia lugha teule na mpangilio fulani wa maneno badala ya kutumia lugha natharia(mflulizo).



Ushairi unaweza kuwa kipera cha fasihi simulizi (nyimbo) na pia katika fasihi andishi kwa sababu mashairi yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya kukariri na pia kwa njia ya maandishi. Mashairi yanayoghanwa badala ya kuimbwa huitwa maghani. 
Uchambuzi
Katika ushairi, tutaangalia:
  • Aina za Mashairi - Kuainisha mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika kila ubeti.
  • Bahari za Ushairi - Muundo wa shairi kulingana vina, idadi ya mizani, vipande, mpangilio wa maneno n.k.
  • Uchambuzi wa Mashairi - Mambo muhimu unayohitajika kuzingatia unapochambua shairi
  • Uhuru wa Mshairi - Ukiukaji wa kanuni za sarufi
  • Istilahi za Kishairi - Msamiati unaotumika katika ushairi km vina, mizani n.k
  • Sifa za Ushairi - Sifa zinazobainisha ushairi kutokana na aina nyingine za sanaa.
  • Umuhimu wa Ushairi - Umuhimu wa ushairi katika jamii.
Istilahi za Kishairi
Haya ni baadhi ya maneno ambayo hautakosa kukutana nayo unapozingatia ushairi. Ni muhimu mwanafunzi kuyajua vizuri.
  • Shairi - ni sanaa ya maneno (utunzi maalum wa lugha ya kisanaa) unaotumia mpangilio na uteuzi maalum wa maneno na sauti ili kupitisha ujumbe fulani.
  • Vina - ni silabi za mwisho katika kila kipande.
  • Mizani - ni idadi ya silabi katika kila mshororo.
  • Mshororo - ni msitari mmoja wa maneno katika shairi.
  • Ubeti - ni kifungu cha mishororo kadhaa.
  • Vipande - ni visehemu vya mshororo vilivyogawanywa kwa alama ya kituo(,)
  • Ukwapi- kipande cha kwanza katika mshororo
  • Mwandamo - Kipande cha tatu katika mshororo
  • Ukingo - kipande cha nne katika mshororo
  • Utao - kipande cha pili katika mshororo
  • Mwanzo - mshororo wa kwanza katika ubeti
  • Mloto - mshororo wa pili katika ubeti
  • Kimalizio/Kiishio - mshororo wa mwisho katika ubeti usiorudiwarudiwa katika kila ubeti.
  • Kibwagizo - mshororo wa mwisho katika ubeti unaorudiwarudiwa kila ubeti.
Sifa za Ushairi
  • Huwa na vina, mizani, mishororo na beti
  • Hutumia lugha teule
  • Hufupisha au kurefusha maneno ili kutosheleza idadi ya mizani
  • Mashairi hayazingatii kanuni za kisarufi. (Angalia uhuru wa mshairi)
  • Hutumia mbinu za lugha
Umuhimu wa Mashairi
  • Kuburudisha
  • Kuhamasisha jamii
  • Kukuza sanaa na ukwasi wa lugha
  • Kuliwaza
  • Kuelimisha
  • Kuonya, kutahadharisha, kunasihi na kuelekeza
  • Kupitisha ujumbe fulani
  • Kusifia mtu au kitu
  • Kukejeli au kukemea mambo yanayoenda kinyume na maadili ya jamii
Aina za Mashairi
BAHARI ZA USHAIRI
Kitengo
Ushairi

Prev
Maghani
Next
Bahari za Ushairi

Mashairi yanaweza kugawanywa katika aina mbalimbali kulingana na idadi ya mishororo katika kila ubeti.
Tanbihi: Aina za Mashairi ni tofauti na Bahari za Ushairi. Aina za mashairi huzingatia idadi ya mishororo katika kila ubeti ilhali Bahari za Shairi hutegemea na muundo wa shairi kwa kuzingatia vina, mizani, vipande na mpangilio wa maneno.
Shairi moja haliwezi kuwa la aina mbili (k.v tarbia na takhmisa) lakini shairi linaweza kuwa katika bahari zaidi ya moja.
Zifuatazo ni aina za mashairi kulingana na idadi ya mishororo katika kila ubeti
AINA
MISHORORO

Umoja/tathmina
1
Tathmina au Umoja ni shairi lenye mshororo mmoja katika kila ubeti.
Tathnia
2
Tathnia ni shairi lenye mishororo miwili katika kila ubeti.
Tathlitha
3
Tathlitha ni shairi lenye mishororo mitatu katika kila ubeti.
Tarbia
4
Tarbia ni shairi lenye mishororo minne katika kila ubeti. Mashairi mengi ni ya aina ya tarbia.
Takhmisa
5
Takhmisa ni shairi lenye mishororo mitano katika kila ubeti.
Tasdisa
6
Tasdisa ni shairi lenye mishororo sita katika kila ubeti.
Usaba
7
Usaba ni shairi lenye mishororo saba katika kila ubeti.
Ukumi
10
Ukumi ni shairi lenye mishororo kumi katika kila ubeti.

Bahari za Ushairi
BAHARI ZA USHAIRI
Kitengo
Ushairi

Prev
Aina za Mashairi
Next
Uchambuzi wa Mashairi

Bahari za ushairi ni nyingi sana. Shairi huainishwa katika bahari fulani kulingana na mtindo wake, umbo lake na matumizi ya lugha.
Mifano ya Bahari za Ushairi
  1. Utenzi - shairi ndefu lenye kipande kimoja katika kila mshororo.
  2. Mathnawi - ni shairi la vipande viwili (ukwapi na utao) katika kila mshororo.
'' Ewe mtunga silabi, na sauti ya kinubi,
Majukumu hatubebi, maadamu hatushibi,
Mateso kwa ajinabi, kwa mabwana na mabibi
Ukija hayatukabi, karibia karibia ''
  1. Ukawafi - ni shairi la vipande vitatu (ukwapi, utao na mwandamo) katika kila mshororo.
'' Nashindwa nikupe nini, nishukuru kwa malezi, mapenzi na riziki,
Ni pendo kiasi gani, lishindalo la mzazi, kweli mama hulipiki,
Ulinilinda tumboni, ukilemewa na kazi, ila moyo huvunjiki,
Kanilisha utotoni, mavazi pia malazi, ukitafuta kwa dhiki.
''
  1. Mavue - Shairi la vipande vinne (ukwapi, utao, mwandamo na ukingo) katika kila mshororo.
'' Sisi walipa ushuru, wajenga taifa, tena kwa bidii, twahangaishwa,
Tumenyimwa uhuru, tuna mbaya sifa, hatujivunii, tunapopotoshwa,
Kila tunapopazuru, damu na maafa, hatutulii, hali ya kutishwa
''
  1. Ukaraguni - shairi ambalo vina vyake vya kati na vya mwisho hubadilika kutoka ubetio mmoja hadi mwingine.
'' Vina Ubeti 1: ---ni, ---mi,
ubeti 2: ---ta, ---lo,
ubeti 3: ---po, ---wa,
''
  1. Ukara - shairi ambalo vina vya kipande kimoja havibadiliki kutoka ubeti mmoja hadi mwingine, lakini vina vya kipande kingine hubadilika. Kwa mfano, vina vya kati vinafanana kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho lakini vina vya kipande cha mwisho vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.
'' vina Ubeti 1: ---shi, ---ma,
ubeti 2: ---shi, ---ko,
ubeti 3: ---shi, ---le,
ubeti 4: ---shi, ---pa
''
  1. Mtiririko - shairi ambalo vina vyake vya mwisho na vya kati havibadiliki kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho.
'' kwa mfano vina vikiwa ( ---ni, ---ka) kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho.
''
  1. Mkufu/pindu - Shairi ambalo neno la mwisho au kifungu cha mwisho cha maneno katika ubeti mmoja, hutangulia katika ubeti unaofuatia.
'' Hakika tumeteleza, na njia tumepoteza,
Nani wa kutuongoza, aliyepewa uweza,
Filimbi akipuliza, tusiyeweza kupuuza,
Bali twaisikiliza, bila ya kuzungumza,

Bila ya kuzungumza, wala mwendo kulegeza,
Tumwandame ja mwangaza, kututoa palipo giza,
Penye dhiki ya kuliza, bila sauti kupaza
Pengo hili kulijaza, ni nani anayeweza, ''
  1. Kikwamba - Neno moja au kifungu cha maneno hurudiwarudiwa kutanguliza mishororo au ubeti katika shairi.
'' Jiwe hili lala nini, ila moshi na majani,
Jiwe linalala lini, litokapo vileoni,
Jiwe hili halineni, lina macho halioni,
Jiwe na tulibebeni, tulitupe mitaroni
''
  1. Kikai - Shairi lenye kipande kimoja kifupi (chenye mizani chache kuliko kingine) Mfano (8,4)
'' Nani binadamu yule, adumuye,
Anayeishi milele, maishaye
Jenezani asilale, aluliye,
Kaburi liko mbele, sikimbiye.
''
  1. Msuko - Shairi ambalo kibwagizo/mshororo wa mwisho ni mfupi kuliko mishororo mingineyo. K.v (8,8) (8,8) (8,8) (8).
'' Hawajazawa warembo, usidhani umefika,
Ukisifiwa mapambo, jinsi ulivyoumbika,
Akipata jipya umbo, 'tabaki kihangaika,
Usidhani umefika. ''
  1. Mandhuma - shairi ambalo kipande kimoja hutoa hoja, wazo ama swali, huku cha pili kikitoa jibu/suluhisho.
  2. Malumbano - Mashairi mawili ambapo mshairi mmoja hutunga shairi akijibu au kupinga utunzi wa mshairi mwengine.
  3. Ngonjera - Shairi lenye wahusika wawili wanaojibizana. K.m. Ubeti wa kwanza, mwalimu, na wa pili, mwanafunzi.
  4. Sakarani - Shairi lenye bahari zaidi ya moja.
  5. Sabilia - Shairi lisilokuwa na kibwagizo. Kituo (mshororo wa mwisho) hubadilika kutoka ubeti hadi ubeti.
  6. Shairi huru - shairi lisilozingatia sheria za ushairi
  7. Shairi guni - shairi lenye makosa ya arudhi za shairi




Uchambuzi wa Mashairi
BAHARI ZA USHAIRI
Kitengo
Ushairi

Prev
Bahari za Ushairi
Next
Maghani

Yafuatayo ni mambo muhimu unayohitajika kuzingatia kila unapochambua shairi.
  1. Muundo/Umbo la shairi
  2. Uhuru wa Mshairi
  3. Maudhui
  4. Dhamira
  5. Mtindo wa / Mbinu za Lugha



Muundo/Umbo la Ushairi
Katika umbo wa shairi, tunaangazia jinsi shairi lilivyoundwa kwa kuangazia mizani, vina, mishororo n.k Aidha, ni muhimu kutaja aina na bahari za shairi zinazohusiana na kila sifa uliyoitaja.
  1. Idadi ya mishororo katika kila ubeti - Tumia idadi ya mishororo kubainisha aina ya shairi hilo. 
Kwa mfano: Shairi lina mishororo minne katika kile ubeti, kwa hivyo ni Tarbia 
  1. Idadi ya mizani katika kila mshororo na katika kila kipande cha mshororo. 
Kwa mfano: Kila mshororo una mizani kumi na sita: nane katika utao na nane katika ukwapi. 
  1. Idadi ya vipande katika kila mshororo - Taja ikiwa shairi lina kipande kimoja, viwili, vitatu au vinne kisha utaje bahari yake.
  2. Kituo, kiishio au kibwagizo - Ikiwa mstari wa mwisho umerudiwa rudiwa, basi shairi lina kibwagizo au kiitikio, la sivyo lina kiishio.
  3. Vina - Zingatia vina vya kati na vya mwisho kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Kisha utaje ikiwa ni Mtiririko, Ukara au Ukaraguni



Uhuru wa Mshairi
Mshairi hafungwi na kanuni za kisarufi za lugha katika utunzi wa shairi. Anaweza kufanya makosa ya kisarufi kimakusudi ili shairi lizingatie umbo fulani. Zifuatazo ni njia mbalimbali ambazo mtunzi wa shairi anaweza kutumia kuonyesha uhuru wake.
  1. Inkisari - kupunguza idadi ya silabi katika neno ili kusawazisha idadi ya mizani katika mshororo.
mfano: kubadilisha nimeona aliyenipenda kuwa meona alenipenda. 
  1. Mazda - kuongeza silabi katika neno ili kusawazisha idadi ya mizani katika mshororo.
mfano: afya ukijaliwa kuwa afiya ukijaliwa . 
  1. Tabdila - kubadilisha silabi ya mwisho ili kustawazisha urari wa vina katika kipande bila kuathiri mizani.
mfano: yahuzunisha dunia kuwa yahuzunisha duniya . 
  1. Kuboronga Sarufi -ni mbinu ya kupangua mpangilio wa maneno ili kuleta urari wa vina au mdundo wa ushairi.
mfano: siku hiyo ikifika kuwa ikifika hiyo siku . 
  1. Utohozi - Kuswahilisha Maneno - Wakati mwingine mshairi anaweza kubadilisha neno la lugha nyingine litamkike kwa Kiswahili ili kudumisha mdundo wa kishairi na pia kupata neno mwafaka litakalotimiza arudhi za kiushairi.
mfano: tukapata intaneti badala ya tukapata 'internet' ama mtandao wa tarakilishi.



Maudhui
Maudhui ni jumla ya ujumbe na mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika shairi fulani. Haya ni mambo yanayotajwa katika hadithi na yanaweza kujumuisha mawazo zaidi ya moja. Maudhui husaidia kujenga dhamira ya shairi.


Dhamira
Dhamira ni lengo, dhumuni au nia ya mtunzi wa shairi. Mtunzi wa shairi anaweza kuwa na kusudi la kutuonya, kututahadharisha au kutunasihi kuhusiana na jambo fulani.



Mtindo wa Lugha
Mtindo wa lugha hurejelea namna mbalimbali ambazo mshairi anatumia mbinu za lugha. Mshairi anaweza kutumia mbinu za lugha. kama vile: Tanakali za Sauti, Istiara, Takriri, Semi n.k



Tamathali za Usemi
TAMATHALI ZA USEMI
Aina
Mbinu/Fani za Lugha
Mbinu za Sanaa
Kiingereza
Figures of Speech

Prev
Ushairi
Next
Fasihi Simulizi

Tamathali za Usemi ni matumizi ya maneno kwa namna fulani ili kuifanya lugha iwe ya kuvuitia na kuifanya kazi ya sanaa iwe ya kupendeza. Kuna aina mbili za tamathali za usemi:
  1. Mbinu au Fani za Lugha- Ni uteuzi wa maneno ili kuifanya lugha iwe ya kupendeza na kuvutia. Pia, Mapambo ya Lugha.
Fani za Lugha zinaweza kutambulikana moja kwa moja bila kusoma kifungu kizima. 
  1. Mbinu za Sanaa- Ni ubunifu wa kisanaa unaojitokeza baada ya kusoma au kusikiliza masimulizi.
Angalau unahitaji kusoma sentensi kadhaa au hata hadithi nzima ili kutambua mbinu ya sanaa iliyotumika. 
Mbinu za Lugha
  • Tanakali za Sauti -Ni mbinu ya kutumia maneno yanayoiga sauti au hali fulani au namna kitendo kilivyofanyika. Milio.
  • Tashbihi -Hii ni mbinu ya lugha inayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha; 'kama', 'mithili ya', 'sawa na', 'ja'. Tashbiha. Similes.
  • Istiara -Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kutumia kiungo 'ni' ama 'kuwa'. Istiari. Sitiari. Imagery
  • Jazanda -
Ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi. 
  • Taashira -Ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika kumaanisha kitu kingine chenye uhusiano na kile kilichotumiwa. Symbolism
  • Taswira -
Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji. 
  • Tashihisi -Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai (sifa za kibinadamu). Uhuishaji. Personification.
  • Chuku -Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe fulani au kusifia kitu. Kutilia Chumvi. Hyperbole
  • Takriri -Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. Repetition
  • Tanakuzi-Tanakuzi ni mbinu ya kusisitiza ujumbe kwa kuambatanisha maneno ya kinyume au yanayokinzana. Ukinzani
  • Majazi -
Majazi ni pale tabia za wahusika zinapoambatana na majina yao halisi. 
  • Lakabu -
Ni mbinu ya mhusika kupewa/kubadikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia/sifa zake. 
  • Semi -
Ni fungu la maneno linapotumika kutoa maana nyingine, badala ya ile ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha ukali wa maneno au kupamba lugha. Kuna aina mbili za semi:
  • Nahau - huwa na vitenzi
  • Misemo - haina vitenzi
  • Methali -
Methali ni misemo ya hekima yenye maana iliyofumbwa. Mhusika, mwandishi wa fasihi anaweza kutumia methali kupitisha ujumbe.
  • Maswali ya Balagha -Tashititi au maswali ya balagha ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika ambayo hayahitaji jibu. Mubalagha. (Rhetorical questions)
  • Uzungumzi Nafsiya -
Mhusika hujizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.
  • Ritifaa -
Mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa (au asiyekuwepo) kana kwamba yuko pamoja nawe.
  • Utohozi -
Kutohoa ni mbinu ya kuswahilisha maneno ya lugha nyingine, yatamkike kama ya Kiswahili.
  • Kuchanganya Ndimi -
Kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili.
  • Kuhamisha Ndimi -
Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu.
  • }
Mbinu za Sanaa
  • Kinaya - Kinaya ni mambo katika sanaa kuwa kinyume na matarajio ya hadhira. Irony
  • Kejeli -Kejeli ni mbinu ya sanaa inayotumia maneno kudharau au kukemea kitendo au mtu fulani.
  • Taharuki -Taharuki ni mbinu ya kusimulia au kuandika riwaya/hadithi kwa kufanya hadhira na/au wahusika wajawe na hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye;
hamu ya kutaka kuendelea kusoma/kusikiliza. Baadhi ya hadithi huishia kwa taharuki na kuilazimisha hadhira yake ijikamilishie au ibaki ikijiuliza maswali. Suspense 
  • Sadfa -
Sadfa ni kugongana kwa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vilikuwa vimepangwa, japo havikuwa vimepangiwa. Coincidence 
  • Kisengere Nyuma -
Mwandishi 'hurudi nyuma' na kuanza kusimulia kisa kilichokuwa kimetendeka kabla ya alichokuwa akisimulia. Aidha, mwandishi hubadilisha wakati wa masimulizi na kuwa wakati wa kisa hicho. Hutumika sana kuonyesha mhusika anapokumbuka kitu, au kutupatia msingi wa jinsi mambo yalivyoanza. Mbinu Rejeshi. Flashback 
  • Kisengere Mbele - Mwandishi anapobadilisha wakati na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni; au kutumia lugha isiyo moja kwa moja kutabiri yatakayojiri. Utabiri. Foreshadow
  • Njozi au Ndoto - Mwandishi hutumia ndoto kutabiri jambo litakalofanyika au kufumbua jambo lililokuwa limefumbwa.
  • Upeo wa Juu - Ni sehemu ya hadithi ambayo matukio yanafanyika kulingana na mapenzi ya hadhira au msomaji. Climax
  • Upeo wa Chini - Ni sehemu ya hadithi ambayo matukio yanafanyika kinyume na mapenzi ya hadhira au msomaji. Aghalabu upeo wa chini hutokea baada ya upeo wa juu. anti-climax
  • Nyimbo - Nyimbo na/au mashairi yanaweza kutumika katika hadithi kwa madhumuni mbalimbali.
Ngano Katika Fasihi Simulizi
HADITHI / NGANO
Utanzu wa
Fasihi Simulizi
Kiingereza
Narratives
Vipera vya Hadithi
Khurafa
Hekaya
Mighani / Visakale
Usuli / Visaviini
Visasili
Ngano za Mazimwi
Ngano za Mtanziko

Prev
Tungo Fupi
Next
Nyimbo

Hadithi (ngano) ni utungo wenye visa vya kubuni unaosimuliwa kwa lugha nathari kwa kusudi la kuburudisha, kukuza maadili na kuunganisha jamii. Msimulizi wa hadithi huitwa Fanani au Mtambaji.
Vipera vya Ngano
Tunaweza kuainisha ngano kulingana na vipengele vifuatavyo:
  1. Wahusika => k.v khurafa, hekaya, mighani, mazimwi,
  2. Maudhui => k.v usuli, visasili, mtanziko
Utanzu huu wa fasihi simulizi umegawanyika katika vipera (aina) kadhaa:
AINA
MAELEZO KWA UFUPI
Khurafa
hadithi ambazo wahusika ni wanyama.
Hekaya
mhusika mmoja (k.v sungura) huwa mjanja kuliko wenzake
Usuli (Visaviini)
huelezea chanzo cha jambo au hali fulani
Visasili
huelezea asili au chimbuko la jamii au mambo ya kiada k.v mauti, ndoa, tohara n.k.
Mighani(Visakale)
hadithi za mashujaa
Mazimwi
huwa na wahusika majitu au mazimwi
Mtanziko
humwacha mhusika katika hali ya kutojua chaguo linalofaa. Kila achagualo lina matukio mabaya.

Sifa za Ngano
  1. Huwa na mianzo maalumu
    1. Paukwa! Pakawa!
    2. "Hadithi! Hadithi!" - "Hadithi Njoo!"
    3. Hapo zamani za kale...
  2. Huwa na miishio maalum
    1. Hadithi yangu yaishia papo!
    2. ...wakaishi kwa raha mustarehe.
  1. Huwa na funzo fulani ambalo aghalabu hutajwa mwishoni mwa hadithi.
  2. Masimulizi yake huwa kwa wakati uliopita
  3. Husimuliwa kwa lugha ya natharia
  4. Huwa na wahusika ambao wanaweza kuwa binadamu, wanyama, miungu, mashetani au vitu visivyo hai
  5. Huhusisha mbinu nyingine za fasihi simulizi kama vile
    1. Nyimbo - kuburudisha, kuamsha hadhira, kupitisha ujumbe
    2. Methali - kutoa funzo
    3. Misemo - kupamba lugha
    4. Vitendawili na mafumbo - kushirikisha hadhira katika masimulizi
  1. Hutumia mbinu ya takriri ili kusisitiza ujumbe kwa kurudiarudia maneno, matukio au nyimbo
  2. Hutumia tamathali za lugha kama vile tashbihi, tashihisi, chuku, tanakali za sauti ili kupamba masimulizi n.k
  3. Huwa na muundo rahisi wenye mwanzo, kati na mwisho.
  4. Ufanisi wake hutegemea mbinu za mtambaji k.v ishara-uso na ubunifu wake jukwaani.
  5. Sehemu fulani zinaweza kubadilishwa kulingana na hadhira
Umuhimu wa Ngano
  1. Kuhifadhi au kurithisha mali ya jamii
  2. Kuunganisha na kukuza ushirikiano miongoni mwa jamii
  3. Kuelemisha au kutoa mafunzo kuhusu mambo fulani
  4. Kukuza maadili mema
  5. Kuonya, kuelekeza, kuhimiza na kunasihi
  6. Kuburudisha hadhira. Hadithi nyingi huwa na visa vya kusisimua na kuburudisha.
  7. Kupitisha muda haswa watoto wanaposubiri chakula kiive
Sifa za Mtambaji wa Hadithi
Msimulizi wa hadithi pia huitwa mtambajifanani au mganaji.
  • Huwa mchangamfu na mcheshi kwa hadhira yake ili kuwafanya wapendezwe na hadithi
  • Anafahamu utamaduni wa jamii yake.
  • Anaifahamu hadhira yake vizuri na kusimulia kulingana na mapendeleo yao. wasichana au wavulana? vijana au wazee?
  • Huwa na uwezo wa ufaraguni - uwezo wa kubadilisha sehemu fulani za sanaa bila kujifunga na muundo asilia.
  • Mwenye kumbukumbu nzuri - uwezo wa kukumbuka
  • Mwenye uwezo wa kuigiza kwa kutumia viungo vyake, uso (ishara-uso) na sauti(kiimbo)
  • Mwenye uwezo wa kujenga taharuki kwa kusita kidogo ili kuvuta nadhari ya hadhira yake.
  • Hushirikisha hadhira yake katika nyimbo n.k
  • Mlumbi hodari na mkwasi wa lugha.

Nyimbo Katika Fasihi Simulizi
NYIMBO
Utanzu wa
Fasihi Simulizi
Kiingereza
Songs



TANZU ZA FASIHI
Prev
Hadithi / Ngano
Next
Maigizo
MBINU ZA SANAA
Prev
Upeo wa Chini
Next
Tanakali

Nyimbo ni aina ya sanaa katika fasihi ambayo hutumia lugha teule, sauti na kiimbo maalum.
Aghalabu nyimbo hutumia ala za mziki kama vile ngoma. Nyimbo zinaweza kuimbwa na mtu mmoja au zaidi.
Wimbo hugawanywa katika beti na mishororo. Nyimbo nyingi huwa na kiitikio au mstari ambao hurudiwa rudiwa.
Sifa za Nyimbo
  1. Hutumia kiimbo au sauti maalum
  2. Huweza kuendamana na ala za muziki
  3. Huimbwa na mtu mmoja au watu wengi; wakati mwingine nyimbo huimbwa kwa kupokezanwa.
  4. Hutumia lugha ya mkato
  5. Hurudiarudia (kukariri) maneno ili kusisitiza ujumbe katika wimbo
Umuhimu wa Nyimbo katika Fasihi Simulizi
  1. Kuburudisha
  2. Kuelimisha, kufunza, kuonya, kuelekeza
  3. Kuliwaza
  4. Kusifia kitu au mtu katika jamii
  5. Kuunganisha jamii
  6. Kudumisha/kuhifadhi tamaduni za jamii
  7. Kukuza talanta na sanaa katika jamii
  8. Hutumika katika mbinu nyingine za fasihi kama vile hadithi
Vipera/Aina za Nyimbo
Kulingana na Muundo:
  • Mashairi
  • Maghani
Kulingana na Ujumbe/Maudhui:
Nyimbo za Ndoa
Nyimbo za harusi huimbiwa bwana na bibi harusi kuwapongeza na kuwapa heko kwa kufunga ndoa yao. Aidha nyimbo hizi huwapa wawili hao mawaidha ya kutunza familia na watoto wao ili waishi pamoja.
Nyimbo za Jandoni/Tohara
huimbwa na vijana wanapopashwa tohara. Nyimbo hizi huonyesha ushujaa, na kuashiria kutoka kwamba anayetahiriwa amekuwa mtu mzima sasa.
Hodiya/Wawe
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa na watu wanapofanya kazi ili kuwatia bidii wafanye kazi bila kuhisi machofu.
Kimai
Nyimbo za Mabaharia - Hizi ni nyimbo za wanabahari wanaposafiri baharini.
Nyimbo za Mazishi/Huzuni/Simanzi
Hizi ni nyimbo za kuliwaza na kuwapa pole walioachwa na marehemu. Nyimbo hizi huwapa matumaini waombolezaji.
Nyimbo za Kidini
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa kumsifia Mungu, kuomba au kutoa mafunzo ya kidini.
Nyimbo za Kisiasa
Hizi ni nyimbo za kuwasifia viongozi wa kisiasa
Nyimbo za Kizalendo
Nyimbo za huonyesha uzalendo kwa kusifia taifa/nchi
Nyimbo za Mapenzi
Katika nyimbo za mapenzi, mwimbaji huimba kwa kumsifia mpenzi wake hasa kwa urembo na tabia zake

Maigizo
MAIGIZO
Utanzu wa
Fasihi Simulizi
Vipera vya Maigizo
Michezo ya Kuigiza
Miviga
Ngomezi
Malumbano ya Utani
Ulumbi
Soga
Vichekesho
Maonyesho ya Sanaa

Prev
Nyimbo
Next
Tungo Fupi

Maigizo ni sanaa katika fasihi simulizi ambayo watendaji huwa ndio wahusika. Maigizo hayasimuliwi kama mbinu nyingine za fasihi. Wahusika ndio huzungumza katika sehemu zao mbalimbali.



Mifano: 
  1. Michezo ya Kuigiza (Jukwaani) - Haya ni maigizo ya jukwaani ambapo watendaji huiga maneno na matendo ya wahusika mbele ya hadhira.
  2. Miviga - Miviga ni sherehe mbalimbali katika jamii fulani. Watu hujumukika na sherehe hizi kulingana na tamaduni zao
  3. Ngomezi - ni sanaa ya ngoma. Midundo mbalimbali ya ngoma hutumika kuwasilisha ujumbe mbalimbali.
  4. Malumbano ya Utani - Malumbano ya utani ni mashindano ya kuongea jukwaani baina ya watu wa makundi au jamii mbili ambayo hutumia kejeli na chuku kukejeli tabia mbaya katika jamii au kundi fulani
  5. Ulumbi - Ulumbi ni uwezo wa kipekee wa kuzungumza mbele ya hadhira. Mtu mwenye uwezo huo wa kipekee wa kuzungumza jukwaani huitwa mlumbi.
  6. Soga - Soga ni mazungumzo baina ya watu wawili au zaidi ambayo aghalabu huwa hayana mada maalum.
  7. Vichekesho - Vichekesho ni aina ya sanaa ya fasihi simulizi ambayo watu hutoa vihadithi vifupi au sentensi zenye uwezo wa kuwafanya wasikilizaji wacheke.
  8. Maonyesho ya Sanaa - Maonyesho huhusisha watu wa jamii au kundi fulani wanaoonyesha taaluma, ujuzi au sanaa yao kwa watazamaji.

Tungo Fupi
TUNGO FUPI
Utanzu wa
Fasihi Simulizi
Vipera vya Tungo Fupi
Methali
Vitendawili
Mafumbo
Semi (Nahau na Misemo)
Vitanza Ndimi na Vichezea Maneno
Lakabu
Misimu

Prev
Maigizo
Maigizo
Hadithi / Ngano

Tungo Fupi ni kipera cha Fasihi Simulizi kinachojumulisha sanaa simulizi zinazoundwa kwa maneno machache; sentensi moja au mbili hivi. Tungo Fupi nyingi huwa na sehemu mbili na aghalabu huhitaji kujibizana ambapo mtu mmoja hutoa pendekezo au swali; halafu mtu mwengine hutoa jawabu - k.m vitendawili na mafumbo. Baadhi ya tungo fupi husemwa na mtu mmoja tu kama vile methali.

Aghalabu vipera vyote vya tungo fupi hutumiwa katika kazi nyingine za fasihi ( na lugha kwa ujumla ) kama mapambo ya lugha.



Vipera vya Tungo Fupi
  1. Methali
    Methali ni tungo fupi za sentensi moja ambazo hutoa funzo fulani kwa njia ya mafumbo. Methali huwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza hutoa hoja nayo sehemu ya pili hutoa suluhisho. Methali hutumika kwa minajili ya kutoa funzo kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Methali nyingine huhitaji hekima ili kujua maana yake.
  2. Vitendawili
    Vitendawili ni tungo fupi ambazo huwa na swali fupi na jibu kwa makusudi ya kupima ufahamu wa hadhira kuhusu mazingira yake. Anayetoa kitendawili huulizia swali lake kwa kutoa maelezo mafupi yanayorejelea umbo la kitu hicho, sauti, harufu au kukifananisha na kitu kingine. Anayejibu huhitajika kufikiria haraka na kutoa jawabu ambalo huwa la neno moja au maneno mawili hivi. Vitendawili huwa na mianzo maalum kulingana na jamii yake.
  3. Mafumbo
    Mafumbo hutumika kuupima uwezo wa mtu kufikira na kufumbua swali ambalo huwa na maelezo marefu. Majibu ya mafumbo huhitaji maelezo na aghalabu hukusudia kujua jinsi mtu anavyoweza kutatua tatizo fulani ambalo linahitaji kufikiria sana.
  4. Vitanza Ndimi
    Vitanza ndimi huwa ni sentensi zinazotumia maneno yanayomkanganya msomaji katika matamshi. Vitanza ndimi huhitaji kutamkwa haraka haraka na kurudiwa rudiwa mara kadhaa kwa kusudi la kukuza uwezo wa kutamka.
  5. Vichezea Maneno
    Ni maneno yanayokaribiana kimatamshi au kimaana hutumika katika sentensi moja kama njia ya kuonyesha ukwasi wa lugha au kuburudisha. Pia hutumika kama vitanza ndimi.
  6. Misimu
    Misimu ni maneno ambayo huzuka miongoni mwa kundi fulani katika jamii na hueleweka tu miongoni mwa watu katika kundi hilo. Misimu hukua na kutoweka baada ya muda.
  7. Lakabu
    Lakabu ni majina yanayobandikwa watu kutokana na sifa zao, maumbile, hulka au mambo yanayowahusu. Lakabu pia ni mbinu ya sanaa.
  8. Semi (Nahau na Misemo)
    Semi ni mafungu ya maneno ambayo hutumika kuleta maana tofauti na maana halisi ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha maneno makali kwa kutumia maneno mengine. Aidha semi zinaweza kutumika tu kwa minajili ya kupamba lugha. Kuna aina mbili za semi: Nahau na misemo

Maghani Katika Fasihi Simulizi
MAGHANI
Kitengo
Ushairi

Prev
Uchambuzi wa Mashairi
Next
Aina za Ushairi

Maghani ni tungo zinazotolewa kwa kughanwa (nusu kuimbwa nusu kukaririwa) Maghani yanaweza kuambatanishwa na ala za muziki au kughanwa kwa mdomo tu.
Aina za Maghani
Zipo fani mbali mbali za maghani ambazo zimeainishwa katika tanzu mbili kuu:
  1. Maghani ya Kawaida
  2. Maghani ya Masimulizi

Maghani ya Masimulizi
Lengo la maghani ya aina hii ni kusimulia kisa fulani, historia, n.k.
Kuna fani mbili za Maghani ya Masimulizi:
a) Tendi
Tendi ni ushairi mrefu unaosimulia matukio ya kishujuaa. Tendi zinaposimuliwa huandamana na ala za muziki.
Sifa za Tendi:
  • Ni ushairi mrefu
  • Husimulia matendo ya kishujaa kwa njia kishairi
  • Husimuliwa badala ya kuimbwa
  • Huandamana na ala za muziki
  • Husimulia visa vya kihistoria
  • Hutungwa papo kwa hapo
b) Rara
Hizi ni hadithi fupi za kishairi zenye visa vya kusisimua, zinazosimuliwa zikiambatanishwa na ala za muziki. Aghalabu hughanwa na watoto; na hutumika kama michezo ya watoto.
Sifa za Rara
  • Ni hadithi fupi za kishairi
  • Husimulia visa vya kusisimua
  • Zinaweza kuimbwa au kusimuliwa
  • Huambatana na ala za muziki
  • Aghalabu huwa ni visa vya kubuni

Maghani ya Kawaida (Sifo)
Maghani ya Kawaida ni maghani yanayosifia mtu, kitu au hali katika jamii
a) Majigambo au Kivugo
Haya ni maghani ambayo mtunzi hujisifia (kujigamba) namna alivyo hodari katika nyanja fulani. Tungo hizi hutumia chuku na maneno ya kejeli kuwadunisha wapinzani wa mtunzi.
Sifa za Majigambo
  • Hutumia nafsi ya kwanza
  • Msimulizi hutumia maneno ya kujigamba
  • Msimulizi hutumia chuku kwa wingi ili kujisifu
  • Hutungwa kwa ubunifu mkubwa na hutumia mbinu kama sitiari, vidokezi, ishara n.k
  • Majigambo mengi huwa mafupi, lakini baadhi yake huwa marefu.
  • Huwa na matendo matukufu ya msimulizi
  • Huwa na ahadi za matendo kutoka kwa msimulizi
b) Tondozi
Tondozi ni aina ya sifo ambayo husifia watu mashuhuri katika jamii kama vile viongozi
Sifa za Tondozi
  • Huwa ni ushairi wa kusimuliwa
  • Husifia mtu mwengine, mtu mashuhuri
  • Hutumia chuku
  • Hutumia mbinu kama sitiari, vidokezi, ishara n.k
  • Hutaja matendo makubwa ya kiongozi anayesifiwa
Pembezi
Pembezi ni maghani ya kumsifu mpenzi.
Sifa za Pembezi
  • Humsifu mpenzi wa mtu
  • Aghalabu huwa ushairi mfupi
  • Hutumia tamathali za lugha kwa wingi kama vile ishara kusimulia umbo la mpenzi
  • Pembezi zinaweza kuandamana na ngoma
ii) Pembezi - tungo za sifa. Zinaweza kusifia kundi fulani la watu, wanyama, njaa, mvua, n.k

Ngano Katika Fasihi Simulizi
HADITHI / NGANO
Utanzu wa
Fasihi Simulizi
Kiingereza
Narratives
Vipera vya Hadithi
Khurafa
Hekaya
Mighani / Visakale
Usuli / Visaviini
Visasili
Ngano za Mazimwi
Ngano za Mtanziko




Prev
Tungo Fupi
Next
Nyimbo

Hadithi (ngano) ni utungo wenye visa vya kubuni unaosimuliwa kwa lugha nathari kwa kusudi la kuburudisha, kukuza maadili na kuunganisha jamii. Msimulizi wa hadithi huitwa Fanani au Mtambaji.
Vipera vya Ngano
Tunaweza kuainisha ngano kulingana na vipengele vifuatavyo:
  1. Wahusika => k.v khurafa, hekaya, mighani, mazimwi,
  2. Maudhui => k.v usuli, visasili, mtanziko
Utanzu huu wa fasihi simulizi umegawanyika katika vipera (aina) kadhaa:
AINA
MAELEZO KWA UFUPI
Khurafa
hadithi ambazo wahusika ni wanyama.
Hekaya
mhusika mmoja (k.v sungura) huwa mjanja kuliko wenzake
Usuli (Visaviini)
huelezea chanzo cha jambo au hali fulani
Visasili
huelezea asili au chimbuko la jamii au mambo ya kiada k.v mauti, ndoa, tohara n.k.
Mighani(Visakale)
hadithi za mashujaa
Mazimwi
huwa na wahusika majitu au mazimwi
Mtanziko
humwacha mhusika katika hali ya kutojua chaguo linalofaa. Kila achagualo lina matukio mabaya.
Sifa za Ngano
  1. Huwa na mianzo maalumu
    1. Paukwa! Pakawa!
    2. "Hadithi! Hadithi!" - "Hadithi Njoo!"
    3. Hapo zamani za kale...
  2. Huwa na miishio maalum
    1. Hadithi yangu yaishia papo!
    2. ...wakaishi kwa raha mustarehe.
  1. Huwa na funzo fulani ambalo aghalabu hutajwa mwishoni mwa hadithi.
  2. Masimulizi yake huwa kwa wakati uliopita
  3. Husimuliwa kwa lugha ya natharia
  4. Huwa na wahusika ambao wanaweza kuwa binadamu, wanyama, miungu, mashetani au vitu visivyo hai
  5. Huhusisha mbinu nyingine za fasihi simulizi kama vile
    1. Nyimbo - kuburudisha, kuamsha hadhira, kupitisha ujumbe
    2. Methali - kutoa funzo
    3. Misemo - kupamba lugha
    4. Vitendawili na mafumbo - kushirikisha hadhira katika masimulizi
  1. Hutumia mbinu ya takriri ili kusisitiza ujumbe kwa kurudiarudia maneno, matukio au nyimbo
  2. Hutumia tamathali za lugha kama vile tashbihi, tashihisi, chuku, tanakali za sauti ili kupamba masimulizi n.k
  3. Huwa na muundo rahisi wenye mwanzo, kati na mwisho.
  4. Ufanisi wake hutegemea mbinu za mtambaji k.v ishara-uso na ubunifu wake jukwaani.
  5. Sehemu fulani zinaweza kubadilishwa kulingana na hadhira
Umuhimu wa Ngano
  1. Kuhifadhi au kurithisha mali ya jamii
  2. Kuunganisha na kukuza ushirikiano miongoni mwa jamii
  3. Kuelemisha au kutoa mafunzo kuhusu mambo fulani
  4. Kukuza maadili mema
  5. Kuonya, kuelekeza, kuhimiza na kunasihi
  6. Kuburudisha hadhira. Hadithi nyingi huwa na visa vya kusisimua na kuburudisha.
  7. Kupitisha muda haswa watoto wanaposubiri chakula kiive
Sifa za Mtambaji wa Hadithi
Msimulizi wa hadithi pia huitwa mtambajifanani au mganaji.
  • Huwa mchangamfu na mcheshi kwa hadhira yake ili kuwafanya wapendezwe na hadithi
  • Anafahamu utamaduni wa jamii yake.
  • Anaifahamu hadhira yake vizuri na kusimulia kulingana na mapendeleo yao. wasichana au wavulana? vijana au wazee?
  • Huwa na uwezo wa ufaraguni - uwezo wa kubadilisha sehemu fulani za sanaa bila kujifunga na muundo asilia.
  • Mwenye kumbukumbu nzuri - uwezo wa kukumbuka
  • Mwenye uwezo wa kuigiza kwa kutumia viungo vyake, uso (ishara-uso) na sauti(kiimbo)
  • Mwenye uwezo wa kujenga taharuki kwa kusita kidogo ili kuvuta nadhari ya hadhira yake.
  • Hushirikisha hadhira yake katika nyimbo n.k
  • Mlumbi hodari na mkwasi wa lugha.

Riwaya
RIWAYA
Utanzu wa Fasihi
Fasihi Andishi
Kiingereza
Novel
Mifano
Kiu, Siku Njema, Mwisho wa Kosa
Angalia
Aina za Wahusika
Hadithi Fupi vs Riwaya

Prev
Tamthilia
Next
Hadithi Fupi

Riwaya ni kazi ya fasihi andishi ambayo huwa ndefu na aghalabu riwaya moja hujaza kitabu kizima. Riwaya huwa na wahusika wengi na huangazia mawazo kadhaa. Aidha, riwaya hufanyika katika mazingira mbalimbali na aghalabu huchukua muda mrefu ikilinganishwa na hadithi fupi.
Aina za Riwaya
Kunazo aina kadhaa za Riwaya katika Fasihi Andishi:
  • Riwaya sahili - visa vyake husimuliwa moja kwa moja na huwa rahisi kueleweka
  • Riwaya changamano - hii ni riwaya ambayo huhitaji kusomwa kwa makini ili kueleweka.
Aghalabu huwa na maudhui mengi na wahusika wengi ambao wanachangia katika tatizo kuu katika riwaya hiyo. Hujengwa kwa taharuki ili kuwavutia hadhira kutazamia jinsi tatizo kuu litakavyotatuliwa. Hutumia mbinu za taharuki na visengere nyuma/mbele. 
  • Riwaya ya kibarua - hutumia muundo wa barua kuwasilisha ujumbe wake.
  • Riwaya kiambo - huhusisha maswala ya kawaida katika jamii



Mifano ya Riwaya
  • Utengano
  • Siku Njema
  • Mwisho wa Kosa
  • Kiu





Tamthilia
TAMTHILIA
Utanzu wa Fasihi
Fasihi Andishi
Kiingereza
Play
Mifano
Mstahiki Meya
Kifo Kisimani
Shamba la Wanyama
Angalia
Wahusika
Michezo ya Kuigiza

Prev
Hadithi Fupi
Next
Riwaya

Tamthilia au tamthiliya ni sanaa ambayo huwasilisha mchezo wa kuigiza kwa njia ya maandishi. Majina ya wahusika huandikwa katika upande wa kushoto, kisha koloni, halafu hufuatiwa na maneno halisi yaliyotamkwa na mhusika huyo.
Aina za Tamthilia
Kunazo aina kadhaa za tamthilia katika fasihi andishi:
  1. Tamthilia Cheshi/Komedia - ni mchezo wa kuchekesha. Maudhui yake huundwa kwa lengo la kutumbuiza hadhira.
  2. Tamthilia Simanzi/Trejedia - ni mchezo uliojaa huzuni, mikasa, mikosi, visa vya kutisha na aghalabu baadhi ya wahusika wakuu hufa.
  3. Tamthilia Simanzi-Cheshi/Trejikomedia - ni mchezo wenye visa vya kuhuzunisha lakini pia unawasilisha kwa njia ya kuchekesha. Aghalabu wahusika hutumia kejeli kuchekesha hadhira ijapokuwa kuna shida fulani inayowakabili. Baadhi ya wahusika wakuu hukumbwa na mikasa.
    Mfano: Kifo Kisimani (na Kithaka Wa Mberia)
  4. Tamthilia Tatizo - ni mchezo wa kuigiza ambapo wahusika huwa na tatizo/shida kuu wanalotaka kulitatua. Tamthilia hii aghalabu hutumia mbinu ya taharuki ili kuwafanya hadhira wawe makini ili kuona jinsi tatizo hilo litakavyoishia.
  5. Tamthilia ya Domestiki Drama - ni mchezo unaoangazia maisha ya kawaida ya watu kama vile familia, urafiki, ndoa n.k
  6. Tamthilia ya Melodrama - ni mchezo ambao husisitiza sifa za wahusika kwa kuunda wahusika kuunda wahusika wenye sifa zilizopigiwa chuku na zisizobadilika. Tamthilia hizi huundwa kwa namna inayowafanya hadhira wawapende wahusika fulani na wawachukie wahusika wengine. Kwa mfano:
    1. Shujaa ambaye hushinda kila mara
    2. Wahusika wabaya ambao hubakia wabaya kutoka mwanzo hadi mwishi
    3. Wahusika wazuri ambao hufanya vitendo vizuri kutoka mwanzo hadi mwisho
    4. Wapenzi ambao hata wakitenganishwa bado watapendana
    5. Aghalabu huishia kwa raha mustarehe
Mifano ya Tamthilia
  1. Kifo Kisimani
  2. Shamba la Wanyama
  3. Mstahiki Meya


Wahusika Katika Fasihi Andishi
WAHUSIKA KATIKA FASIHI ANDISHI
Kiingereza
Characters
Angalia
Tamthilia
Hadithi Fupi
Riwaya

Fasihi Andishi hutumia wahusika wanadamu, kinyume na Fasihi Simulizi ambayo hutumia wahusika changamano (watu, wanyama, mazimwi n.k). Kunazo aina kadhaa za wahusika katika kazi ya fasihi andishi kama vile: tamthilia, riwaya na hadithi fupi.
Aina za Wahusika
  1. Wahusika Wakuu Ã¢‡’ hawa ni wahusika ambao wanahusishwa na takribani visa vyote katika riwaya/tamthilia. Wahusika huhusishwa kutoka mwanzo hadi mwisho.
Aghalabu mhusika mkuu hafi isipokuwa katika trejedia/simanzi au hufa kifo cha ushujaa. 
  1. Wahusika Wasaidizi Ã¢‡’ hawa ni wahusika wanaosaidia kujenga mhusika mkuu. Hutokeza mara nyingi katika hadithi.
Wahusika wasaidizi wanaweza kuwa na visa vyao. Kwa mfano marafiki na aila za wahusika wakuu. 
  1. Wahusika Wadogo Ã¢‡’ ni wahusika ambao wanafanya kazi ndogo sana katika fasihi kama vile kujenga maudhui au mandhari. Wahusika hawa wakitolewa,
riwaya/tamthilia inaweza kuendela bila kubadilika sana. Kwa mfano mwenye duka ambalo mhusika alinunua kitu fulani. 
  1. Wahusika Bapa Ã¢‡’ hawa ni wahusika wasiobadilika kutoka mwanzo hadi mwisho. Kwa mfano, mhusika mbaya anabakia kuwa mbaya kutoka mwanzo hadi mwisho.



Sifa za wahusika bapa huweza kutambulika mwanzoni mwa hadithi/riwaya. Wahusika bapa hawawakilishi sifa halisia za binadamu. Nia yao ni kujenga tabia moja tu.
Kuna aina mbili za wahusika bapa:
    1. Wahusika bapa-sugu - huoenyesha msimamo wao kulingana na masimulizi ya msanii.
    2. Wahusika bapa-vielelezo - msimamo wao hutambulika kulingana na majina yao. Msanii hutumia mbinu ya majazi au lakabu kuwapatia wahusika majina yanayolingana na sifa zao.
Kwa mfano: Mhusika Rehema ni mwenye huruma na neema kutoka mwanzo hadi mwisho. 
  1. Wahusika Duara Ã¢‡’ mhusika duara hubadilika kitabia katika fasihi. Hawana msimamo thabiti. Hubadilika kulingana na maudhui na mazingira. Kwa mfano, msichana aliyeanza kama mpole na mwadilifu anapobadilika na kuwa mtovu wa nidhamu, kahaba na asiyeshirikiana na mtu yeyote.
  2. Wahusika Wafoili Ã¢‡’ huwa katikati ya wahusika bapa na wahusika duara. Wanaweza kuchukua msimamo fulani katika maswala fulani lakini pia wanaweza
kubadilisha msimamo huo wakati mwingine kulingana na hali. Wahusika hawa hutegemea wahusika duara na wahusika bapa ili kutoa sifa zao. Kwa mfano, wakiishi na mhusika bapa, wanaweza kuchukua msimamo wa mhusika huyo lakini wakikaa sana na mhusika mwengine, wanabadilika. Wahusika hawa aghalabu huwakilisha uhalisi wa binadamu. 



VITENDAWILI

Vitendawili ni tungo fupi ambazo huwa na swali fupi lisilo wazi na jibu kwa makusudi ya kupima ufahamu wa hadhira kuhusu mazingira yake. Anayetoa kitendawili huulizia swali lake kwa kutoa maelezo mafupi yanayorejelea umbo la kitu hicho, sauti, harufu au kukifananisha na kitu kingine. Anayejibu huhitajika kufikiria haraka na kutoa jawabu ambalo huwa la neno moja au maneno mawili hivi. Vitendawili huwa na mianzo maalum kulingana na jamii yake.
--------------------------------------------------------------------------------

Sifa za Vitendawili

1.Vitendawili huwa na mwanzo maalum : Kitendawili – tega
2.Hupitishwa baina ya watu wawili – anayetega na anayetegua
3.Vitendawili huwa na muundo maalum wa kuendelezwa (utangulizi, swali, (majaribio ya) jibu; wanaotegua wakishindwa anayetega huwa ameshinda, huitisha apewe mji/zawadi na kisha kutoa jibu)
4.Huwa na vipande viwili – swali na jibu. Mfano: Kila niendapo ananifuata – kivuli.
5.Hutumia mbinu ya jazanda, kufananisha vitu viwili moja kwa moja. K.v. Nyumba yangu haina mlango – yai (yai limelinganishwa moja kwa moja na nyumba isiyo mlango)
6.Hurejelea vitu vinavyopatikana katika mazingira na vinavyojulikana sana
7.Vitendawili vilitegwa wakati maalum, hasa wa jioni
8.Vitendawili hutumia tamathali za usemi (mbinu za lugha) kama istiara, tashihisi, tashbihi, jazanda, chuku, tanakali za sauti, n.k
9.Vitendawili huwa na jibu maalum.

---------------------------------------------------------------------------

Aina za Vitendawili

a) Vitendawili sahili

ni vifupi na huwa na na muundo mwepesi kueleweka. K.v.
b) Vitendawili mkufu

huwa na vipande vinavyofuatana na kila kipande huwa na uhusiano na kipande kilichotangulia. Mfano – nikisimama anasimama, nikiketi anaketi, nikiondoka huondoka pia
c) Vitendawili vya tanakali

hutumia tanakali za sauti Mfano: Drrrrrrh mpaka ng’ambo – buibui; huku ng’o na kule ng’o.
d) Vitendawili sambamba

huwa na maelezo marefu (kama hadithi fupi) halafu jibu lake huwa ni refu pia (kama mafumbo)
----------------------------------------------------------------------------

Umuhimu wa vitendawili

1.Vitendawili huburudisha kwani hutegwa kwa njia ya uchangamfu na ushindani.
2.Huwaleta watu pamoja (huunganisha jamii) kwani vinapotegwa watu hukusanyika pamoja.
3.Vitendawili huhamasisha watu kuhusu mazingira yao kwani hulenga vitu vinavyopatikana katika jamii hiyo.
4.Vitendawili hukuza uwezo wa kufikiria/kukumbuka kwani anayetoa jibu huhitajika kukumbuka jibu la kitendawili.
5.Vitendawili hukuza na kuhifadhi tamaduni kwa maana hupokezanwa kutoka kizazi hadi kizazi.
6.Vilitumika kupitisha wakati na kuwafanya watoto wasilale mapema kabla ya chakula kuwa tayari.