Kiswahili sanifu kidato cha tano

 

Hiki ni kitabu kipya kilichoandaliwa kwa ajili ya wanafunzi na waalimu wa Kiswahili
kidato cha tano katika shule za sekondari.Ni cha kukidhi haja ya muhtasari wa sekondari
nchini Rwanda.Hii ina maana kwamba maelezo yote kuhusu somo hili yatakayotolewa
humu yatakuwa ni yale yanayolingana na kidato hiki.
Kitabu hiki kimeandikwa na Bwana NIYIRORA Emmanuel na
NDAYAMBAJE Ladislas, kutoka Chuo Kikuu cha Elimu cha Kigali (KIE). Kitabu hiki
kitawasaidia wanafunzi kujua lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya kibantu na iliyopiga
hatua kimatumizi, kimsamiati, na yenye kutumiwa na jamii mbalimbali barani Afrika na
ulimwengu kwa ujumla