Kiswahili sanifu kidato cha nne

 

Kitabu hiki ambacho ni “Kitabu cha mwanafunzi kidato cha nne” kinaundwa na
sehemu kuu 6 ambazo ni: historia ya Kiswahili, fasihi, ngeli za majina, usemi halisi
na usemi wa taarifa, utungaji na aina za maneno. Kitabu hiki kitasaidia katika
ufundishaji wa Kiswahili katika shule zinazofundisha lugha kikiwemo Kiswahili.
Kitatilia mkazo matumizi ya Kiswahili katika maisha ya kila siku kwa wale wanaohitaji
kuelewa na kutumia Kiswahili ipasavyo.
Kitabu hiki kimeandikwa na NDAYAMBAJE Ladislas na NIYIRORA Emmanuel ambao
ni walimu kutoka Chuo Kikuu cha Elimu cha Kigali. Ndani mwake tulitoa maelezo ya
kila mada inayounda kitabu hiki pamoja na mazoezi yatakayowafanya wanafunzi
kukua kiakili na kijamii