Kiswahili - Lugha na Sarufi kidato cha Tano na Sita

Kitabu hiki cha Kiswahili Sckondari Kidato cha lano na Sita • Lugha na Sarufi kinajumla ya sura tisa. Sura hizo ni 

  1. Matumizi ya lugha, 
  2. Maendeleo ya Kiswahili, 
  3. Kukua na kuenea kwa Kiswahili, 
  4. Sarufi ya Kiswahili, 
  5. Tungo za Kiswahili, 
  6. Utungaji, 
  7. Ufahamu naufupisho, 
  8. Tafsiri na ukalimani, na 
  9. Makosa katika matumizi ya lugha.

Kitabu hiki kimezingatia Muhtasari wa Somo la Kiswahili kidato cha Tano na Sita wa mwaka 2009. Mada zote zimefafanuliwa kwa kina na zinamshirikisha mwanafunzi kikamilifu. Maswali ya mazoezi na tamrini yameandaliwa kwa lengo la kumfikirisha na kumjengea mwanaftinzi umahiri katika somo. Hali kadhalika. lugha iliyotumika katika kitabu hiki ni rahisi, na itakayomwezesha mwanafunzi kujifunza somo la Kiswahili vizuri.

Kimeandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania